← Back to News

254 CHRONICLES

254 CHRONICLES
Oginga Odinga Alikua Kinga

Oginga Odinga alikua kinga...
So nikimuimba nadai kuringa.

Alikua na utu ambao time ya ukoloni ulishika kutu...
Wakoloni walimuona worthy, watu wakamuona holy.

But alikataa kuform serikali na siety wakoloni walikua wakali...
All KANU wanted was Mzee apate kibali.

1963 si tulikua free...
Mungu alitumwagia baraka...
Mjaluo na mkikuyu waliweza kuitana kaka,
chuki tukapiga kiraka.

Wakati Kenyatta alipata,
siezi sema kwa Kenyatta umoja haukua hoja,
cause I believe Harambee ilikua ili bendera yetu ipepee....

1978 no debate, Moi ka president.
Wakati Moi alipata, wengi hawakua walala hoi,
maziwa si mlikunywa na sieti toka Ziwa Victoria.

Kwa education hawakulia...
maziwa every week, so they were never weak.

Sec. 2A ikawa repealed juu wengi walililia haki,
so come 2002 tulililia haki na Kibaki hakubaki,
si alitupakilia free education ikakuja,
wengi wakaikubalia na sisi tukailaki.

Sisemi 2007 hatungeweza fika heaven...
Sisemi 2007 Mr. X hakuchukua state...
Wengi walidhani amekunja mkia,
but katiba ndio tupate tiba aliichangamkia...
Si devolution ikakuja but baada ya damu kuvuja.

2013 wakati Uhuru alipata,
si Uhuru tulipata...
But siezi sema kwa nini niliskia some parts wakipiga nduru.

Does it mean hawakua huru
ama donda la 2007 halikua limepona?

Sauti Sol walikuja na call tujiangalie,
but badala ya kusoma barua tuliirarua,
na I believe haikua fault ya Karua.

2017 wakati NASA iliapisha, siku expect Miguna angejinasa.
Mnakumbuka waki-mprovoke,
I never knew citizenship by birth inaeza kuwa revoked.

2022 nashangaa walifikaje chuo kikuu
na hesabu ya 1+1 iliwachenga.

Maybe the DJ should start from scratch
ndio tujue ni wapi tulikua na option ya kuruka mavi,
tukadecide turuke mkojo,
but tukaland kwa shit.

Sai praise opposition uambiwe Sifu
na uende.

Next time mnafaa kuvote na akili,
stori na kitendawili mligundua ni nyinyi mnajitega.

By The Poet Dan.

Published

Sep 07, 2026

Status

Published

Related News