Katika dunia ya leo, taarifa husafiri kwa kasi kuliko hapo awali. Kwa kubofya kitufe kimoja tu, ujumbe unaweza kuwafikia maelfu ya watu ndani ya dakika chache. Lakini si kila taarifa tunayoiona kwenye simu au mitandao ya kijamii ni ya kweli.
(Misinformation) ni taarifa isiyo sahihi inayosambazwa bila kujua na mara nyingi huwa haina madhara makuu. Mtu anaweza kushiriki habari kwa sababu anaamini ni kweli, kumbe amepotoshwa. Kwa upande mwingine, (disinformation) ni taarifa za uongo au zilizopotoshwa zinazotengenezwa na kusambazwa kwa makusudi ili kudanganya, kuchochea hofu au kuathiri maamuzi ya watu.
Tatizo kubwa ni kwamba sote tunaweza kuwa sehemu ya mnyororo huu bila kujua. Wakati mwingine tunaposoma kichwa cha habari, tunakasirika au kufurahi, kisha tunashiriki bila hata kuthibitisha chanzo. Sekunde chache za kutafakari zinaweza kuzuia taarifa ya uongo kuwafikia mamia ya watu.
Katika zama hizi za kidijitali, kabla ya kusambaza taarifa, tujiulize: Chanzo chake ni kipi? Ni kweli? Taarifa hii inaweza kumdhuru mtu au jamii? Na je, kuna vyanzo vingine vinavyoithibitisha?
Kupambana na (misinformation na disinformation) si jukumu la waandishi wa habari pekee. Ni jukumu letu sote. Kuthibitisha kabla ya kushiriki ni hatua ndogo, lakini inaweza kuwa mchango mkubwa katika kujenga jamii yenye taarifa sahihi, yenye utulivu na inayoweza kufanya maamuzi kwa uelewa.